Password Must Contain / Neno la siri lazima lijumuishe
* 7 to 15 characters / herufi 7 mpaka 15
* at least one numeric digit / angalau tarakimu 1
* at least one special character / angalau herufi 1 ya kipekee
Mambo Muhimu ya kuzingatia wakati wa ujazaji fomu
Mwombaji anatakiwa kuwa na anuani ya barua pepe ambayo ataitumia kujisajili na kupokea kiunga kitakachomuwezesha kukamilisha usajili wake.
Mwombaji anatakiwa kuwa na nyaraka zisizopungua mbili zitakazotumika kuthibitisha utambulisho wake. Mfano, cheti cha kuzaliwa na nyinginezo.
Mwombaji anatakiwa kufanya “scanning” ya nyaraka hizo na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja kwa kila kiambatisho) au picha katika muundo wa JPG au PNG.
Ni muhimu Mwombaji kujaza Namba ya simu ya mkononi.
Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha Kuzaliwa endapo amezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea. Aidha, endapo Mwombaji amezaliwa kabla ya mwaka 1980 anatakiwa kuambatisha cheti cha Kuzaliwa au “Affidavit”.
Kwa Waombaji wenye majina mengine; ni vyema kuandika majina hayo ili endapo ikatokea uhitaji wa kurekebisha majina yake iwe rahisi kutambulika.
Mwombaji anatakiwa kujua majina ya Baba na Mama yake mzazi.
Mwombaji ambaye ana Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi wake; anatakiwa kuwa na viambata halisi (kwa wazazi waliokwishapata vitambulisho vya Taifa).
Mwombaji anatakiwa kujua namba ya Nyumba, Mtaa na kata anayoishi.
Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi, wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi katika Nchi husika kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ili kujaza sehemu ya makazi, Mtaa/Kata kwa usahihi.
Endapo Mwombaji ana vyeti vya Shule, TIN na Kadi ya mpiga kura, ni vyema kuambatanisha.
Mwombaji anatakiwa kujaza Fomu kwa usahihi na kuhakikisha viambata vyake na taarifa alizo jaza hazikinzani na taarifa za shule au Biashara.
Mwombaji anatakiwa kufika katika Ofisi ya NIDA iliyoko kwenye Wilaya yake ya makazi akiwa na Fomu iliyokamilika (Fomu iliyogongwa Mhuri na kuwekwa Saini ya Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa), pamoja na nakala za viambatisho vyake alivyopakia katika mfumo wakati wa usajili ili kukamilisha taratibu za usajili.
Kwa Mwombaji mwenye uhitaji wa kupata maelezo ya ziada; asisite kufika katika ofisi ya NIDA iliyopo katika Wilaya yake.